Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:53

Ujumbe wa UM wa Liberia wapongezwa


UNMIL
UNMIL

Naibu wa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa umoja huo nchini Liberia, UNMIL, anasema ujumbe huo umefanya kazi nzuri ya kuleta usalama kwa taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kipindi cha vurugu, na kwamba sasa ni wakati mwafaka kwa nchi hiyo kuwajibika kwa usalama wake.

Mnamo mwaka wa 2003, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 1509 lililoiunda UNMIL, ambayo pamoja na majukumu mengine, ilitarajiwa kuwalinda raia wa Liberia na kusaidia serikali ya nchi hiyo kubuni na kutekeleza mikakati ya mageuzi ya usalama wa kitaifa.

Wajibu wa UNMIL ulimalizika tarehe 30 mwezi uliopita, na kwamba ujumbe huo uliwasilisha rasmi majukumu ya kiusalama kwa Liberia.

Naibu huyo wa mwakilishi Maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, WALDEMARD VREY, anasema kuwa UNMIL haina jukumu la kulinda usalama lakini itaendelea kuwepo nchini Liberia na kuunga mkono serikali ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG