Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 15:32

UNITAID inazindua juhudi za kufadhili matibabu ya TB


Pini inayosomeka "Stop TB" imeoneshwa baada ya ripoti ya WHO juu ya TB huko Geneva.

Taasisi ya kimataifa ya UNITAID inauchukulia kwa dhati msemo wa zamani kuwa ni vyema kuzuia kuliko kutibu.

Mkurugenzi mtendaji, lelio Marmora ameiambia Sauti ya Amerika-VOA kuwa taasisi yake inajitayarisha kutumia kati ya dola milioni 40 na 80 kwa mapendekezo ambayo yanaweza kutoa matibabu rahisi ya muda mfupi na gharama nafuu kwa watu ambao wako katika hatari ya kupata kifua kikuu.“Marmora anasema tunachotamani ni kuwa na orodha ndefu ya miradi na kuona jinsi miradi hii inavyoweza kufanya kazi kusini mwa afrika na eneo la afrika magharibi ambaloo wanazungumza kifaransa, eneo la sahel, na pengine asia, na huko Latin amerika itategemea”.

Kifua kikuu kinaambukiza sana kwa njia ya hewa ni maradhi ambayo yanaua kiasi cha watu milioni moja na nusu kila mwaka. Shirika la afya duniani-WHO linakadiria kwamba theluthi moja ya idadi ya watu dunaini wana virusi vya kifua kikuu, hivyo wanajulikana kuwa ni wabebaji wa virusi hivyo lakini hawana maradhi na havijakuwa na uwezo wakuambukiza.

Picha ya kitabibu ikionesha pafu lililoathirika kwa TB. Jan, 2014.
Picha ya kitabibu ikionesha pafu lililoathirika kwa TB. Jan, 2014.

Kiasi cha asilimia 15 ya watu wenye dalili za virusi hivi wanatarajiwa baadaye kuugua kifua kikuu. Makundi mawili ambayo yako katika hatari zaidi inasema WHO ni watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano na watu wanaoishi na HIV.

Matibabu kwa TB ni marefu. Yanawataka wagonjwa kunywa dawa za vidonge kila siku kati ya kipindi cha miezi sita na 36. Mkurugenzi wa program ya Global TB katika WHO, Mario Raviglione anasema uamuzi wa UNITAID kuwekeza katika matibubabu ya kuzuia ni hatua kubwa sana katika kuelekea katika kumaliza TB ifikapo mwaka 2030.

“Ravigilione anasema anadhani itakuwa ni mabadiliko ya msingi kwasababu ni mara ya kwanza wanaona hatua za kweli katika kiwango cha ufadhili kama huu, kutumia nyenzo za kifedha kama hivi ni moja ya njia ya kweli ya kusonga mbele. Na kuongezea hii itakuwa na mchango mkubwa katika kuzuia mamilioni ya watu kuugua kifua kikuu pamoja na kuepuka vifo kwasababu mara unapozuia unakuwa huna maradhi na kunakuwa hakuna vifo”.

Mkurugenzi wa program ya Global TB katika WHO, Mario Raviglione.
Mkurugenzi wa program ya Global TB katika WHO, Mario Raviglione.

Raviglione anasema ana matumaini ufadhili wa UNITAID utaisukuma sekta ya utengenezaji madawa kutengeneza dawa bora, rahisi na ambazo zinaweza kutumika katika kipindi cha muda mfupi ili kuzuia kifua kikuu.

XS
SM
MD
LG