Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 00:44

UNISFA yalaani harakati za watu wenye silaha katika  sehemu ya kusini mwa Abyei


Mji wa Abyei

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Abyei (UNISFA) uililaani harakati za watu wenye silaha katika  sehemu ya kusini inayojulikana kama Boksi la Abyei siku ya Jumatano.

Wakati wanajeshi wakiendelea kuonekana, Ujumbe huo una wasiwasi mkubwa kwamba maendeleo haya ya hivi karibuni katika sehemu ya kusini ya Abyei yatazidisha mzozo katika eneo hilo na kusababisha mateso yasiyoelezeka na wasiwasi wa kibinadamu kwa raia katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ujumbe huo ulibainisha kuwa Boksi la Abyei unasalia kuwa eneo lisilo na silaha ambalo halipaswi kuwa na nguvu yoyote iwe ya kawaida au yenye silaha ya jumuiya zote mbili. Kwa hivyo ni muhimu kwamba wote waheshimu maazimio husika ya Baraza la Usalama katika suala hili.

UNISFA ililaani mapigano mapya ndani na nje ya mipaka ya eneo hilo na kuzitaka pande zote kusitisha mapigano na kuruhusu mchakato wa kisiasa kusuluhisha mzozo unaoendelea. Wanasisitiza kuwa ni kinyume cha aina yoyote ya upelekaji wowote wa wanajeshi usioidhinishwa ndani ya eneo hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG