Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 07:25

UNICEF na WFP zasaidia waathirika wa ukame Somalia


Mashirika mawili ya kimataifa ya misaada yanaongeza juhudi kusaidia wakazi wa eneo lililokubwa na ukame la kaskazini mwa Somalia.

Idara ya watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) zinasema zinatoa msaada wa haraka wa kibinadamu kwa ajili ya kuokoa maisha huko Somaliland na Puntland.

Maeneo hayo yana utawala wake ndani kaskazini magharibu na kaskazini mashariki mwa Somalia.

Hali ya ukame imesababisha idara hizo mbili kutoa msaada wa chakula, mipango ya virutubisho vya mwili, huduma za afya na msaada pamoja na upatikanaji wa maji safi na kuboresha hali ya huko.

UNICEF na WFP zinakadiria wakazi 385,000 wanahitaji msaada wakati wengine milioni 1.3 wnaweza kuingia katika mgogoro endapo hali ya ukame itaendelea na msaada utachelewa kuwasili.

XS
SM
MD
LG