Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:33

UNHCR yahofia kuongezeka dharura ya kibinadamu Ethiopia


Eneo lenye vita huko Tigray Ethiopia
Eneo lenye vita huko Tigray Ethiopia

Wakati shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR linasema Alhamisi linahofia kuongezeka kwa dharura ya kibinadamu miongoni mwa raia wanaolazimika kukimbia mapigano kati ya wanajeshi wa shirikisho na vikosi vya ndani katika mkoa wa Tigray, kaskazini mwa Ethiopia. 

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa mashambulizi ya anga na vita vimeuwa mamia, vimepelekea wakimbizi kufurika nchini Sudan, vimechochea mgawanyiko wa kikabila nchini Ethiopia na kuuliza maswali juu ya sifa ya Abiy, kiongozi kijana zaidi wa Afrika, aliyeshinda tuzo ya Nobel mwaka 2019.

Mkoa wa magharibi wa Tigray umekombolewa, aliandika Abiy, mwenye umri wa miaka 44 kutoka kabila kubwa la Oromo, na aliyewahi kupigana na wa-Tigray dhidi ya nchi jirani ya Eritrea.

Jeshi sasa linatoa misaada ya kibinadamu na huduma nyingine. Pia linatoa chakula kwa watu, ameongeza Abiy.

Lakini Ann Encontre, mwakilishi wa UNHCR nchini humo aliliambia shirika la Habari la Reuters, kwamba nchi jirani ya Sudan, tayari imepokea zaidi ya wakimbizi 10,000 wa Ethiopia tangu mapigano yalipoanza.

Mwakilishi wa UNHCR, Ethiopia anaeleza : "UNHCR tayari imeona huko Sudan, mashariki mwa Sudan, kuwasili kwa watu kutoka Tigray wanaotafuta hifadhi. Watu elfu saba wamewasili wakiwa na hali mbaya sana katika siku tatu zilizopita na tuna wasi wasi sana kwamba mashambulizi yanayoendelea, mashambulizi ya jeshi na mapigano, watu wengi wanazidi kukimbia wakiwemo wakimbizi ambao wapo katika kambi na watu wengine. Wanaweza kutafuta usalama wao nchini Sudan."

Encontre pia alisema kuwa mkoa huo unapungukiwa chakula, mafuta na bidhaa nyingine za msingi. Alionya kuwa mzozo huo ulifungua uwezekano wa manyanyaso ya kingono kwa wanawake na watoto.

Alisema UN inashauriana juu ya fursa ya kuwafikia watu wote wanaohitaji msaada na imeomba msaada wa kufikisha mahitaji kwa watu hao, jambo ambalo Encontre, alisema ni vigumu kwa sababu wanahitaji kushughulika na serikali za kieneo pamoja na Addis Ababa.

"Wazee ambao hutegemea watu wengine kwa misaada ya kawaida ya kibinadamu. Kuandikisha Watoto kutoka kwenye kambi na maeneo mengine ili kujiunga na jeshi wakati wanapopigana. Na pia kuhakikisha kwamba tunaweza kuendeleza juhudi zetu za kibinadamu kuwapatia msaada wakimbizi, wanaotafuta hifadhi, ambao wanatuangalia sisi kuwapatia misaada," amesema mwakilishi huyo wa UNHCR.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema Alhamisi kwamba jeshi la taifa, limepata miili ya wanajeshi wake ambao walikuwa wamefungwa kamba na kupigwa risasi huko Tigray.

Ahmed hakusema ni miili mingapi iliyopatikana na hakuna maoni ya haraka kutoka chama tawala huko Tigray cha TPLF.

Mawasiliano yamedhoofika huko Tigray, tangu mzozo ulipoanza.

Abiy anaishutumu TPLF kwa kuanzisha mzozo na kushambulia kambi ya jeshi la serikali na kukaidi mamlaka yake, wakati wa-Tigray wakisema utawala wake wa miaka miwili umewatesa.

XS
SM
MD
LG