Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 11:18

Abiy amfukuza mkuu wa jeshi na maafisa wa ngazi za juu Ethiopia


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alimbadilisha mkuu wa jeshi lake Jumapili, huku wanajeshi wengi wakiripotiwa kujeruhiwa katika mzozo wa siku tano katika mkoa wa kaskazini wa nchi hiyo wa Tigray.

Mshindi huyo wa Tuzo ya amani ya Nobel wakati huo huo alitaka jamii ya kimataifa ielewe operesheni ya kijeshi aliyoanzisha wiki hii dhidi ya chama cha Tigray, ambacho ameshutumu kwa kutaka kuleta hali ya ukosefu wa uthabiti katika taifa hilo.

Abiy alisema chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) kilichokuwa kinatawala zamani kilikuwa kimefadhili, kufundisha na kuandaa jeshi lolote ambalo lilikuwa tayari kushiriki katika vitendo vya vurugu na haramu ili kukomesha mpito wa kidemokrasia ambao ameufuata.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG