Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 12:51

UNESCO yatoa ripoti ya malengo bora ya elimu kwa mtoto ifikapo 2030


 Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Viashiria vilivyotumika kuamua mafanikio ya nchi shiriki vilihusisha mahudhurio ya elimu ya utotoni, viwango vya kuacha shule, viwango vya kumaliza shule, mwanya wa  jinsia katika viwango vya wanaomaliza shule, viwango vya chini vya ustadi katika kusoma na hisabati, na matumizi katika elimu ya umma.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumatatu ilisema dunia inashindwa kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 watoto wote wanapata elimu bora inayojumuisha na inayolingana na fursa za kujifunza maishani.

Viashiria vilivyotumika kuamua mafanikio ya nchi shiriki vilihusisha mahudhurio ya elimu ya utotoni, viwango vya kuacha shule, viwango vya kumaliza shule, mwanya wa jinsia katika viwango vya wanaomaliza shule, viwango vya chini vya ustadi katika kusoma na hisabati, waalimu waliopatiwa mafunzo, na matumizi katika elimu ya umma.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilisema nchi tayari zinashindwa kuwasaidia watoto wao hata kabla ya kuzingatia matokeo yanayotokana na COVID-19 katika maendeleo ya elimu. Kushindwa huku ni mwamko kwa viongozi wa ulimwengu ripoti ya UNESCO ilisema kwani mamilioni ya watoto wataendelea kukosa shule na masomo ya hali ya juu.

Vigezo vya elimu vimejumuishwa katika lengo la nne la maendeleo endelevu, moja ya malengo 17 yaliyowekwa mwaka 2015 na baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Malengo yanakusudiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2030.

XS
SM
MD
LG