Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:32

UNAIDS: Maelfu ya watoto wanakufa kutokana HIV na ukimwi


MIchel Sidibe Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS akizungumza na Msani Theron.
MIchel Sidibe Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS akizungumza na Msani Theron.

Program ya Ukimwi ya Umoja wa Mataifa inasema maelfu ya watoto wanakufa kutokana HIV na Ukimwi, kinyume na watu wazima, hawapatiwi tiba kwa ugonjwa huu ambao unasababisha vifo.

HIV na Ukimwi si tena ni kifo tu. Watu walioambukizwa ugonjwa wanaweza kuishi maisha ya kawaida, ili mradi tu wanapatiwa matibabu na huduma, bahati mbaya, kuna tofauti kubwa sana ya dhahiri kati ya jinsi watoto na watu wazima wenye HIV na Ukimwi wanavyotibiwa.

Msemaji wa UNAIDS Charlotte Spector anasema asilimia 76 ya watu wazima wana fursa ya matibabu lakini ni nusu tu ya watoto wanaoishi na HIV wanapatiwa matibabu ya kuokoa maisha. Anasema watoto ni asilimia 15 ya vifo vyote vitokanavyo na Ukimwi, licha ya kuwa ni asilimia nne ya watu wote wanaoishi na ugonjwa huu.

“Mwaka jana pekee watoto 160,000 waliambukizwa HIV. Kwa hiyo, kinachotokea ni kwamba nchi 12 zilikuja pamoja barani AFrika kwasababu nchi sita kusini mwa jangwa la Sahara barani humo zinawakilisha asilimia 50 ya wale wenye maambukizi mapya,” alisema Spector.

Anasema ushirika wa ulimwengu ulioongozwa na UNAIDS, Shirika la Afya Duniani na UNICEF uliundwa ili kuufunga mwanya mkubwa. Anasema nchi 12 za kiafrika zimeungana katika ushirika huo. Spector anasema mawaziri wa afya kutoka nchi nane watazindua juhudi hizo wiki ijayo nchini Tanzania.

Spector anasema, “kwahiyo, siyo tu kuwapata watoto ili kuwapatia matibabu, lakini lililo muhimu ni kujaribu kusitisha maambukizi yanayojulikana kama ‘Vertical Transmission.’ Sasa nini hasa ni ‘Vertical Transmission?’ Ni mama kumuambukiza HIV wakati wa uja uzito, wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha kwa sababu maambukizi mengi yanatokea wakati wa kunyonyesha.”

Spector anasema juhudi za kudhibiti kusambaa kwa HIV barani Afrika chini ya jangwa la Sahara zimejikita zaidi katika kuwapatia watu wazima matibabu, ambao ni wasambazaji wakuu wa virusi. Katika utaratibu huo, hata hivyo, anasema mahitaji ya watoto hayakuangaliwa.

“Kwa hiyo kinachotokea ghafla ni kwamba imebainika kuwa tumewasahau hawa watoto, na kuna kizazi kilichosahauliwa cha watoto. Kwahiyo sasa, kumekuwepo na jitihada za kulifunga hilo bomba, kama naweza kusema, ni kuwafikia watoto kabla ya hata kuzaliwa au baada ya kuzaliwa,” anasema Spector.

Ushirika wa ulimwengu utaendesha program hii kwa miaka minane ijayo mpaka mwaka 2030. Wakati wa kipindi hicho, inalenga kuondoa mwanya wa matibabu kwa waja wazito na wasichana wanaonyonyesha na wanawake wanaoishi na HIV, kuzuia na kutambua maambukizi mapya ya HIV, kutoa fursa ya upimaji na matibabu, na kumaliza vikwazo vya kijamii ambavyo vinazuia fursa za upatikanaji wa huduma.

XS
SM
MD
LG