Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:51

Unachotakiwa kujua kuhusu Brexit


Bendera ya Uingereza ikionekana chini huko London siku moja baada ya kura ya kujitoa kwenye EU. June 24, 2016.
Bendera ya Uingereza ikionekana chini huko London siku moja baada ya kura ya kujitoa kwenye EU. June 24, 2016.

Nini maana ya “Brexit”. Ni kifupi cha maneno ambayo yanamaanisha uwezekano wa Uingereza kujitoa kutoka ndani ya nchi 28 zilizo katika umoja wa ulaya-EU. Lilifuata mfano wa “Grexit” lililotumiwa wakati Ugiriki ilikuwa karibu kutolewa katika matumizi ya sarafu ya Euro.

June 23 wapiga kura wa Uingereza walipiga kura ya kujitenga kutoka EU.

Swali la Kura ya maoni: Wapiga kura waliulizwa, “ Inafaa Uingereza iendelee kubaki kuwa mwanachama wa EU au iondoke kutoka EU? Swali lilipendekezwa na tume ya uchaguzi ya Uingereza na kukubaliwa na serikali pamoja na bunge la nchi hiyo.

Brexit Baltics
Brexit Baltics

Kwa nini sasa: Ili kukamilisha matakwa ya Conservative Party na kudumaza wapinzani wa EU, Waziri Mkuu wa uingereza, David Cameron aliahidi kufanya kura ya maoni kama angechaguliwa tena mwaka 2015. Wa-Conservative ambao hivi sasa ndio wengi wamegawanyika juu ya swali la uanachama wa EU kwa takribani miaka 40. Wa-Conservative wa hali ya chini kwa jumla wanapendelea kuondoka EU.

Umuhimu: Watu waliopendekeza Uingereza kujitoa wanaamini itaipa uhuru Uingereza kutoka utawala ambao unazuia mafanikio ya uundwaji wa ajira na kuruhusu nchi kuchagua sheria yake na marafiki wa biashara. Wanaharakati wa Uingereza wanaounga mkono uanachama wa Uingereza katika jumuiya kama ambavyo zilivyo nchi nyingine itasaidia kuboresha ushawishi wa nchi ulimwenguni katika masuala ya jeshi na usalama wa kiuchumi.

Wapigakura wanaostahiki: Raia wa Uingereza wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ndio waliopiga kura. Hii inajumuisha raia huko Uingereza na katika mataifa ya jumuiya ya madola.

Muda gani itachukua kuondoka EU: Mara sheria namba 50 itakapoanza kazi ambapo ni rasmi inaeleza nia ya kuondoka, muda wa miaka miwili unaanza kutumika. Katika kipindi hicho Uingereza itaendelea kukubaliwa na mkataba pamoja na sheria za EU, lakini haitashiriki katika kufanya maamuzi yeyote.

Maduka ya fedha ulimwenguni yalishuka kufuatia Brexit.June 24, 2016
Maduka ya fedha ulimwenguni yalishuka kufuatia Brexit.June 24, 2016

Nini kitatokea wakati wa kipindi hicho? Uingereza itaanza kuzungumzia vipengele vya kuondoka kwake. Masuala makubwa sana ikiwemo vitu kama kanuni gani za kifedha ambazo bado zitakuwepo kwa mji wa London, ushuru wa biashara na haki za makundi ya raia kwenye mataifa ya umoja wa ulaya.

Athari gani zinazoonekana kwa Uingereza kujitoa umoja wa ulaya? Baadhi wanaamini kujitoa uanachama wake kutahamasisha mataifa mengine kufuata mfumo wa kufanyika kura ya maoni kwenye maeneo yao.

XS
SM
MD
LG