Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:52

UN yasema uchaguzi lazıma ufanyike Afrika ya Kati ifikapo Disemba 27


Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema Jumuiya ya Kimataifa ina amini kwamba ni lazima uchaguzi ufanyika nchini humo hapo Disemba 27.

Pia amesema kuwa UN inalaani harakati zozote za kuzuia taifa hilo kuendelea mbele na mpito mpya wa kisiasa.

Wito huo umetolewa wakati waasi wanaripotiwa wameuteka mji wa Bambari, uliyoko magharibi mwa nchi hiyo hapo Jumanne.

Mashambulio hayo ya Jumanne yanafuatia tuhuma zilizotolewa mwishoni mwa wiki na serikali ya Bangui kwamba Rais wa zamani Francois Bozize anapanga njama pamoja na makundi ya waasi yenye silaha kuipindua serikali kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumapili.

Kulingana na Abel Matchipata Meya wa Bambari mji wa nne kwa ukubwa ni kwamba mji huo uko chini ya udhibiti wa makundi yenye silaha na afisa mmoja wa serikali amethibitisha kwamba mji umetekwa na wanasubiri msaada wa kijeshi.

Akizungumza na waandishi habari kupitia mtandao mwakilishi maalum wa Karibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya umoja huo nchini humo Mankeur Ndiaye amesema jeshi la UN nchini humo MINUSCA, liko imara na lina mamlaka kamili ya kutumia nguvu kwa ushirikiano na jeshi la taifa, ili kuwaruhusu wapiga kura kutoka na kushiriki kwenye uchaguzi kwa uhuru na amani.

Ndiaye Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema : "Jumuiya ya kimataifa inaamini kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike Disemba 27 ili kuheshimu utaratibu uliowekwa na katiba. Hii leo vifaa vyote vya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Bunge vimewasilishwa katika majimbo kwa msaada wa MINUSCA, ili kuweza kukamilisha matayarisho ya uchaguzi."

Kuna kikosi cha kulinda amani cha UN nchini humo cha MINUSCA chenye wanajeshi elfu 11 500. Siku ya Jumamosi serikali iliyatuhumu makundi matatu ya waasi yanayo ungwa mkono na Rais wa zamani Francois Bozize kuanza mashambulizi kuelekea mji mkuu wa Bangui.

Kutokana na hayo Rais Faustin-Archange Touadera aliomba Russia na Rwanda kupeleka wanajeshi zaidi. Russia ilitangaza jana kwamba imepeleka wakufunzi wa kijeshi 300, Na Rwanda ilipeleka wanajeshi wake siku ya Jumatatu.

Faustin-Archange Touadera, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anaeleza : "Kile tunacholaani ni kwa watu kuzusha ghasia badala ya kuingia kwenye utaratibu, ili tuweze kupata amani, chini na mpango wa kidemokrasia kwa vile hivi sasa tuna mfumo wa utawala wa kikatiba . Ni lazima tudumishe utulivu kwa ajili ya demokrasia nchini mwetu."

Makundi hayo matau yanaolaumiwa kuzusha mapigano mepya yaliunga muungano wa wazalengo wanaotaka mageuzi CPC, na kutyataka makundi mengine ya waasi kuungana nao.

Hali hii yote imezusha wasiwasi na hasira miongoni mwa wananchi. Akizungumza na shirika la AFP Lucie Abatumu Profesa katika kitengo cha sayansi katika chuo kikuu cha Bangui anasema wamechoshwa na vita.

Lucie Abatumu, Profesa kaika chuo kikuu cha Bangui anaeleza : "Je, kwa hakika unaweza kujenga nchi kupitia vita. Kwa maoni yangu haimkiniki. Ikiwa kuna matatizo hebu tukae kwenye meza na kuyajadili na kutafutia suluhisho. Na wakati wamajadiliano ni lazima kila upande ukubali kuweza kushinda na pia kuweza kushindwa."

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kimataifa, ICC, Fatou Bensouda alitoawa wito jana wa kuwepo utulivu ili kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa amani.

Taifa hilo la Afrika ya kati lilitumbukia katika vita vya kidini mwaka 2012 kufuatia kupinduliwa kwa Francois Bozize. Maelfu ya watu waliuliwa na watu milioni 4.5 kukimbia. Tangu 2018 juhudi za kurudisha utawala wa kidemokrasia zimekuwa zikiendelea kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG