Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:17

UN yasema takriban watu 7 wameuwawa DRC


Waandamanaji wakiwa katika eneo la kanisa DRC
Waandamanaji wakiwa katika eneo la kanisa DRC

Vyombo vya ulinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) vimewauwa siyo chini ya watu saba waliokuwa wakiandamana kumtaka Rais Joseph Kabila kujiuzulu, walinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) wamesema.

Polisi Jumatatu wamesema watu watatu walikufa na vifo viwili kati ya hivyo vinachunguzwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC wanaharakati wa Kanisa na vyama vya upinzani walikuwa wameunga mkono maandamano hayo.

Katika makubaliano yaliyofikiwa mwaka mmoja uliopita, Rais Kabila alikuwa tayari amekubali kujiuzulu ifikapo mwisho wa mwaka 2017.

Hatua hiyo ilikuwa mwaka mmoja baada ya kumaliza awamu yake ya pili katika nafasi hiyo. Lakini uchaguzi wa kumtafuta mrithi wake hivi sasa umeahirishwa mpaka Disemba 2018.

Wanaharakati wa Kikatoliki walikuwa wametaka kuwepo maandamano baada ya ibada ya Jumapili, lakini serikali ya Congo ilipiga marufuku maandamano hayo.

Polisi walitumia risasi na mabomu ya machozi kuzuia waandamanaji kukusanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya kanisani.

Watu wawili walipigwa risasi na kuuwawa nje ya kanisa katika mji mkuu wa Kinshasa, Kikundi cha Human Rights Watch kimesema.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa (UN) Florence Marchal amesema kuwa pamoja na watu hao saba waliouwawa kwa kupigwa risasi mjini Kinshasa, muandamanaji mwengine aliuwawa katika mji wa Kananga.

Zaidi ya watu 120 walikamatwa, amesema.

XS
SM
MD
LG