Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:41

UN yapeleka timu A. magharibi kukabiliana na uharamia


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, bwana Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, bwana Ban Ki-moon

Umoja wa Mataifa umepeleka timu yake nchini Benin kukabiliana na uharamia unaoleta kitisho kwenye kanda hiyo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amepeleka timu Afrika magharibi kutathmini na kupendekeza mpango bora wa kukabiliana na uharamia katika ghuba ya Guinea.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa anasema katibu mkuu, Ban Ki-Moon, alipeleka timu hiyo nchini Benin, kufuatia ombi la Rais Boni Yayi. Timu hiyo pia itatembelea Nigeria, Gabon na Angola.

Mwezi uliopita, bwana Ban alihimiza kuwepo idara za usalama na sheria katika nchi za ghuba ya Guinea, kuungana pamoja kupambana na ugaidi huku wakilinda maendeleo ya uchumi na usalama wa kanda hiyo. Baraza la usalama pia limepitisha azimio linalohimiza mataifa katika ghuba ya Guinea kuitisha mkutano wa viongozi juu ya namna ya kukabiliana na kitisho cha uharamia.

Maharamia wamekuwa wakifanya mashambulizi katika ghuba ya Guinea na kufanikiwa mara kwa mara wakilenga meli zinazobeba mafuta kutoka eneo la kusini mwa Nigeria la Delta.

Mwezi June idara ya kimataifa inayoshughulika na masuala ya majini ilitoa onyo moja la uharamia kwa meli zinazosafiri karibu na Benin.


XS
SM
MD
LG