Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:48

Serikali na upinzani Sudan Kusini wahimizwa kutekeleza ahadi za mkataba wa amani


Raia walopoteza makazi yao nchini Sudan Kusini

Takriban miaka miwili ya mapigano baina ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makam rais wake wa zamani Riek Machar, yamewafanya zaidi ya watu millioni 2.3 kupoteza makazi yao. Hiyo inajumuisha takriban raia elfu mia 180 waliobanduliwa kutokana na ghasia na ambao walikuwa wakihifadhiwa katika kambi sita za umoja mataifa kote nchini humo.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:22 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Baraza la usalama la umoja mataifa limethibitisha tena utayari wake hapo jana wa kuchukuwa hatua dhidi ya wale wanaovuruga utaratibu wa amani nchini Sudan kusini na wale ambao wanawanyanyasa raia na kushambulia walinda amani.

Balozi wa Marekani kwenye umoja mataifa, Samantha Power, ambaye ni rais wa sasa wa baraza hilo alisema kuwa wamejadili haja ya pande zote kwenye mzozo kushiriki kikamilifu kwa niaya dhati ya kusitisha mapigano na utaratibu wa amani, na kadhalika kuunda serikali ya mpito, bila ya kucheleweshwa Zaidi.

Akizungumza kwa wadhifa wake wa kitaifa Bi Power alisema wote serikali na upinzani lazima waonyeshe nia ya dhati na azma ya kisiasa ili kuhakikisha makubaliano hayasambaratiki.

Mkuu wa walinda amani katika umoja mataifa Herve’ Ladsous, aliliambaia baraza kuwa utaratibu wa amani wa sudan kusini uko katika wakati muhimu.

Anasema maendeleo ya kutekeleza mpango wa amani wa Agasti 26, umekuwa wa kasi ya pole pole na kudumazwa na matatizo mazito akirejea kuelezea kuhusu ukiukaji wa makubaliano ya sitisho la mapigano yaliyofikiwa na pande zote hususan upande wa jimbo la unity. Ladsous anasema ukiukaji huu umesababisha kiwango kikubwa cha watu kupoteza maisha yao, na kupoteza makazi yao na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.

Umoja mataifa una vikosi na polisi takriban elfu 13 nchini Sudan kusini. Mkuu huyo wa walinda amani anasema vikosi ziada elfu moja mia moja vinahitajika kutowa ulinzi, lakini pia navyo havitoshi.

Ladsous anasema hakuna kiwango cha vikosi au polisi kitakachoweza kuchukuwa nafasi ya nia ya kisiasa inayohitajika kutoka kwa viongozi wa Sudan kusini kumaliza mzozo wao.

Baraza la usalama la umoja mataifa lazima liamuwe ifikapo December 15 juu ya mabadiliko ya mamlaka ya sasa ya vikosi vilivyopo ili kuweza kusaidia kutekeleza mpango wa Amani na kulinda raia.

Balozi wa Sudan kusini kwenye umoja mataifa Francis Deng, alirudia ahadi ya rais Kiir ya kutekeleza makubaliano. Anasema serikali imeanza kuondowa wanajeshi wake hadi kilomita 25 nje ya mji mkuu Juba, kama ilivyo agizwa kwenye makubaliano.

Takriban miaka miwili ya mapigano baina ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makam rais wake wa zamani Riek Machar, yamewafanya zaidi ya watu millioni 2.3 kupoteza makazi yao. Hiyo inajumuisha takriban raia elfu mia 180 waliobanduliwa kutokana na ghasia na ambao walikuwa wakihifadhiwa katika kambi sita za umoja mataif akote nchini humo.

XS
SM
MD
LG