Umoja wa Mataifa unasema matatizo ya chakula nchini Somalia yanaongezeka haraka kufuatia kupanda kwa bei za vyakula na ukame unaoendelea katika eneo hilo.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia, Mark Bowden, alionya Jumatano kwamba watu wengi huwenda wakafariki kutokana na utapiamlo, kama hakuna kitakachofanywa kuzungumzia tatizo hili.
Bowden alisema bei za vyakula nchini Somalia zimepanda hadi asilimia 270 ukilinganisha na mwaka mmoja uliopita, kwa sababu ya ukame wa muda mrefu kote pembe ya Afrika.
Alisema Somalia inapok
ea kiasi cha asilimia 40 pekee ya msaada wa kimataifa ilioomba. Mkuu wa program ya chakula duniani ya Umoja wa Mataifa alisema Jumatano kuwa shirika hilo linapunguza program zake nchini Somalia na Ethiopia kwa sababu ya kuzorota kwa rasilimali.
Josette Sheeran alisema watu milioni 10 katika eneo hilo wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.
Umoja wa Mataifa karibuni ulisema pembe ya Afrika inataabika na ukame mbaya katika muda wa miongo sita.