Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:47

Umoja Mataifa waridhishwa na juhudi za malengo ya SDG


Naibu katibu mkuu wa Umoja Mataifa Bw. Jan Eliasson.
Naibu katibu mkuu wa Umoja Mataifa Bw. Jan Eliasson.

Umoja Mataifa umeridhishwa na juhudi za ulimwengu zinazoendelea za kutekeleza malengo endelevu ya maendeleo ambayo mataifa yaliahidi kutekeleza ili kuboresha maisha ya raia wake.

Mwezi September mwaka jana, viongozi 190 wa dunia waliahidi kutekeleza malengo enedelevu ya mendeleo 17 ili kumaliza umaskini uliokithiri, kurekebisha mabadiliko ya hali ya hewa na kupambana dhidi ya ukosefu wa usawa, vilevile na dhulma, katika juhudi za kupata ulimwengu uloshamiri, ulokuwa na usawa na ambao ni endelevu. Malengo ya SDG yanadhamiriwa kuchochea hatua katika kipindi cha miaka 15 ijayo katika maeneo ya umuhimu mkubwa.

Katika mahojiano maalum na sauti ya America, naibu katibu mkuu wa Umoja Mataifa Jan Eliasson, alielezea matumaini juu ya jinsi malengo ya SDG yanatekelezwa kitaifa na kuwa kweli , kimkakati na kimipango.

Eliasson anasema tayari wameanza kuyatekeleza malengo katika kiwango cha kitaifa. Huu ni mwaka wa kwanza, na ni mwezi wa pili na tayari tuna takriban mataifa 25 ambayo yanataka kutueleza ifikapo kipindi cha msimu wa joto tutakapokuwa na mkutano mkubwa juu ya utekelezaji, kile wanachokifanya.

Bw Eliasson anasema kupitia malengo ambayo yanahusu kila mtu, na yanapaswa kukubaliwa na wote na kutekelezwa na wote, watu masikini na matajiri. Yamejengwa juu ya uwendelevu wake, kuwa kwa kuunganisha ajenda ya malengo endelevu ya maendeleo na ajenda ya mabadiliko ya hali ya hewa. Yote yanaingiliana, na lazima yamfikie kila mtu, na lazima tuwe na ari ya kupambana na ukosefu wa usawa na kuwafikia wale walio nyuma, tusimwache yeyote nyuma, tunasema huu ni ujumbe wa umoja.

Bw Eliasson alisema malengo yanaathirinkila sekta za serikali na jamii na hayawezi kufanikiwa bila kulenga dhana zote jinsi serikali inavyoweza kujipanga, ikiwa ni pamoja na mifumo ya usafiri, miundo mbinu ya kilimo, kiviwanda, uhamiaji na ukuwaji wa miji miongoni mwa mambo mengine.

Hata hivyo wafatiliaji wanasema, mizozo inayoendelea huwenda ikahujumu juhudi za kutekeleza malengo ya SDG hususan barani Afrika.

Eliasson anasema mojawapo ya changamoto za kutekeleza SDG ni ukosefu wa data zinazohitajika kufanikisha malengo ambayo nchi inakabiliana nayo.

Anasema timu za Umoja Mataifa ziko tayari kusaidia mataifa kutekeleza malengo ya SDG.

XS
SM
MD
LG