Katika ripoti yake mpya, UNODC inasema matumizi ya cocaine yameongezeka barani Afrika na Asia, kadhalika katika masoko yanayofahamika huko Ulaya na mabara ya Amerika.
Inasema kilimo cha Koka Amerika Kusini kiliongezeka kwa asilimia 35 kati ya 2021 na 2022. UNODC imeongeza kuwa muongo mmoja uliopita ulishuhudia vitovu vipya vya ulanguzi wa cocaine vikiibuka Afrika magharibi na Afrika ya kati.
Mkuu wa UNODC, Ghada Waly, amesema uwezekano wa soko la cocaine kupanuka barani Afrika na Asia ni jambo linaloonekana wazi na la hatari.
Facebook Forum