Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 20:53

UN inatarajia muongozo wa Taliban kuruhusu wanawake kufanyakazi


Mkuu wa idara ya masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, katikati.

Mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, Jumatatu amesema kwamba anatarajia orodha ya miongozo kutoka serekali ya Taliban kuruhusu wanawake kufanyakazi.

Kufanya huko kazi ni katika sekta ya misaada ya kibinadamu, kufuatia marufuku ya mwezi uliopita ya kuwakataza kufanyakazi.

Martin Griffiths aliwaeleza wanahabari akiwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, kufuatia ziara ya wiki iliyopita mjini Kabul akiwa na viongozi wa mashirika kadhaa ya misaada ya kimataifa.

Hapo Desemba 24, Taliban ilitangaza marufuku ya wanawake wa Afghanistan kufanyakazi katika mashirika ya ndani na kimataifa ya misaada na kusababisha mashirika yasiyo ya kiserekali ya kimataifa kusitisha kazi zao.

Griffthis akiwa na afisa mwandamizi wa UNICEF, shirika la Marekani la the Save the Children, katibu mkuu wa Care International walikwenda Kabul, wiki iliyopita kukutana na maafisa wa juu wa Taliban.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG