Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:44

UN imeomba dola milioni 460 kukabiliana na mafuriko Pakistan


Watu wahama maeneo yaliyokumbwa na mafuriko huko Pakistan
Watu wahama maeneo yaliyokumbwa na mafuriko huko Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewahimiza wafadhili kuharakisha misaada kwa waathiriwa wa mafuriko makubwa ya maji nchini Pakistan

Viongozi wa Pakistan wanasema kwamba mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini mwao yamevuruga maisha ya takriban watu milioni 20. Maji ya mafuriko kutokana na mvua za monsoon yamegharikisha malefu ya vijiji na miji na kuosha barabara kuu na madaraja, mazao na mifugo.

Umoja wa Mataifa umeomba dola milioni 460 kwa ajili ya misaada ya haraka baada ya mafuriko, ikisema mabilioni ya dola yanahitajika kwa muda mrefu ujao ili kuwasaidia waathirika wa mafuriko kurejea katika maiusaha yao ya kawaida.

Katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa Ban Ki-moon amesema ziara yake kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko huko Pakistan ilikua na lengo la kutoa masikitiko yake na mashikamano wa Umohja wa Mataifa kwa wote, serikali na watu wa Pakistan.

"Niko hap pia kuihimiza Jumuia ya kimataifa kuharakisha misaada kwa watu wa Pakistan." Aliwambia waandishi habari kuwa ataripoti kwenye mkutano mkuu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi ambao utajadili mahitaji ya Pakistan na msaada unaohitajika,

Marekani tayari imetoa zaidi ya dola milioni 76 za msaada na imepeleka helikopta kusaidia katika juhudi za misaada huko Pakistan.

XS
SM
MD
LG