Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:50

Guterres aapishwa kuwa Katibu mkuu wa UN


Antonio Guterres akiapishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jumatatu Dec 12, 2016.
Antonio Guterres akiapishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jumatatu Dec 12, 2016.

Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa Jumatatu kuwa katibu mkuu wa 9 wa Umoja wa Mataifa.

Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa Jumatatu kuwa katibu mkuu wa 9 wa Umoja wa Mataifa. Wakati akihutubia mataifa wanachama, Guterres alisema Umoja wa Mataifa lazima uwe wenye kutekeleza majukumu yake kwa wakati. Amesema Umoja huo lazima pia uangazie maswala yanayohusu watu kabla ya kuzingatia zaidi mikakati.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 67 na aliewahi kuwa waziri mkuu 1995- 2002 na pia kiongozi wa shirika la kushughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2005- 2015, alishinda wagombea wenzake zaidi ya darzeni moja kwenye mchujo wa uchaguzi uliochukua miezi 10.

Gueterres anakabiliana na kibarua kigumu wakati ulimwengu ukishuhudia tatizo la uhamiaji, mapigano kwenye mashariki ya kati na Afrika, ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi atakapochukua usukani Januari mosi kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja huo anaeondoka Ban Ki –moon.

XS
SM
MD
LG