Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 03, 2022 Local time: 23:53

UN yasema zaidi ya watu 1,000 waliuwawa nchini Ivory Coast


UN yasema zaidi ya watu 1,000 waliuwawa nchini Ivory Coast

Umoja wa Mataifa unasema watu wasiopungua 1,000 waliuwawa huko magharibi mwa Ivory Coast wakati wa miezi mitano ya matatizo ya kisiasa nchini humo.

Afisa mmoja wa haki za binadamu katika tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo, Guillaume Ngefa, amesema Alhamis kwamba watu wasiopungua 500 waliuwawa katika mji wa Duekoue. Idadi hiyo ni chini ya kiasi cha watu 300 walioripotiwa na wafanyakazi wa kutoa msaada.

Baadhi ya mapigano makali yalitokea huko Duekoue, wakati majeshi yanayowatii marais wapinzani Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara walipokuwa wakipigania madaraka. Wapiganaji kutoka pande zote wanashutumiwa kwa mauaji na kuwabaka raia.

XS
SM
MD
LG