Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:48

Mwakilishi wa umoja mataifa Congo asihi uchaguzi kufanyika kwa wakati.


Mwakilishi maalum wa umoja mataifa nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Martin Kobler
Mwakilishi maalum wa umoja mataifa nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Martin Kobler

Martin Kobler, anasema mvutano wa kisiasa unazidi kuongezeka kabla ya tarehe iliyopangwa ya kufanyika uchaguzi wa bunge na wa rais nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, hapo Novemba 2016.

Mwakilishi wa Umoja wa Matifa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, anaemaliza mhula wake anaihimiza serikali ya Kinshasa kuchukua hatua zote muhimu ili kuhakikisha kwamba uchaguzi wa kitaifa unafanyika kwa wakati mwezi ujao na kuwa wa uwazi, wa haki na kujumuisha watu wote.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Alionya kwamba ukiukaji wa haki za binadamu unaongezeka kukiwepo zaidi ya visa 2,200 vya ukiukaji vilivyoripotiwa mwaka huu na kuathiri zaidi ya watu 5000. Amesema vyombo vya serikali vimehusika na nusu ya ukiukaji huo.

Kobler amekua akisimamia kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani huko Congo chenye wanajeshi elfu 22, tangu Agosti 2013.

Mwanadiplomasia huyo ameisihi serikali ya Congo kufanya kazi na Umoja wa Mataifa juu ya mkakati wa kuondoka kwa awamu ya walinda amani nchini humo, akisema “hatuwezi, na haijabidi, kuondoka kwa haraka”.

XS
SM
MD
LG