Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:07

Umoja Mataifa yaendelea na juhudi za kutatua mzozo wa walopoteza makazi Congo


Wanawake walopoteza makazi huko Congo
Wanawake walopoteza makazi huko Congo

Ukosefu wa uthabiti katika nchi jirani kumewalazimisha maelfu ya watu kutafuta hifadhi nchini DRC.

Umoja wa Mataifa unaripoti kuwa, juhudi zingali zinaendelea kumaliza mzozo wa muda mrefu wa watu walopoteza makazi yao huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kwa kutafuta masuluhisho muafaka kwa mamillioni ya watu walopoteza makazi.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inabaki kuwa na mzozo wa mda mrefu wa kibinadam barani Afrika, huku mizozo ikiendelea huko Kivu kusini na kaskazini, jimbo la Ituri na Katanga kaskazini.

Ukosefu wa uthabiti katika nchi jirani kumewalazimisha maelfu ya watu kutafuta hifadhi nchini DRC. Idara ya kuhudumia wakimbizi ya umoja mataifa inaripoti kuwa kulikuwa na zaidi ya watu millioni 2.5 walopoteza makazi yao, na zaidi ya wakimbizi laki moja nchini DRC mwishoni mwa waka jana.

Mamadou Diallo, mratibu wa masuala ya kibinadam katika umoja mataifa, anasema mda umechelea wa kumaliza mzozo huu.

Bw. Diallo anasema, sasa wameanza majadiliano na serikali ya Congo kujadili suala la suluhisho la kudumu kwa tatizo la ukosefu wa makazi, kama njia ya kuhakikisha kuwepo kwa njia salama ya kurejea kwa watu walopoteza makazi kwenye maeneo walokuwepo awali, au kutafuta suluhisho jengine la kudumu kwa kuwapatia makazi mepya au kuwarejesha baadhi ya watu walopoteza makazi katika jamii zitakazowapokea , kama njia ya kumaliza mzozo huo wa watu kupoteza makazi yao kwa mda mrefu.

Umoja wa mataifa umezindua ombi la msaada wa dola millioni mia 690 kusaidia watu takriban millioni 7 huko DRC, ambao Zaidi ya nusu yao, wanaathiriwa na njaa. Vipao mbele ni pamoja na mifumo ya humda za afya, maji na vyoo, na kadhalika msaada kwa mamillioni ya waahiriwa wa ubakaji na uhalifu wa ngono na usaidizi kwa wale walopeteza makazi.

Diallo, hata hiyo anasema taifa hilo, hususan mashariki mwa Congo, lina uwezo mkubwa wa kiuchumi, kukiwa na amani.

Ameiambia Sauti ya America kuwa Kivu ya kaskazini na kusini, ambayo ni mchangiaji mkuu wa chakula nchini congo zina uwezo wa kulisha taifa zima, na kuuza mazao yao kwa nchi jirani.

Bw. Diallo anasema, kwa vile kuna ukosefu wa usalama, watu walopoteza makazi, baadhi yao hawana tena uwezo wa kurejea kwenye mashamba yao, na kuhudumia mazao yao na kufanya mambo mengine. Kwa hiyo, wanabakia ndani ya kambi na kutegemea misaada.

Diallo anasema hali inaweza kubadilishwa kwa nia ya kisiasa kutoka serikalini, na rasli mali zinazohitajika kusaidia mamillioni ya watu walopoteza makazi, kuacha maisha ya kutegemea misaada na kurejelea maisha ya kawaida.

XS
SM
MD
LG