Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:26

Guterres ateuliwa rasmi kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa


Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Umoja wa Mataifa Alhamisi umemteua rasmi waziri mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres kuwa katibu mkuu wake.

Umoja wa Mataifa Alhamisi umemteua rasmi waziri mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres kuwa katibu mkuu wake. Guterres atachukua nafasi ya katibu mkuu wa sasa Ban ki-Moon ambaye muda wake unamalizika mwisho wa mwaka huu.

Ban ameshikilia wadhifa huo kutoka mwaka wa 2005 hadi 2015. Guterres mwenye umri wa miaka 67 alikuwa waziri mkuu wa Ureno kuanzia 1992 hadi 2002. Vile vile aliwahi kuongoza shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi tangu mwaka wa 2005 hadi 2015.

Katika mahojiano na VOA wakati wa kampeni yake, Guterres alisema kuwa anawania nafasi ya juu ya umojawa mataifa kwasababu alitaka kuweka mazingira ya kusuluhisha changamoto zinazokabili ulimwengu.

Wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepongeza uteuzi wa Guterres huku balozi wa Russia kwenye Umoja huo Vitaly Churkin akisema Guterres ni chaguo bora.

“ ni mwanasiasa wa ngazi ya juu. Amekuwa waziri mkuu wa nchi yake. Ni mtu ambaye anazungumza na kila mtu,anamsikiliza kila mtu,anazungumza ukweli, ni mtu muwazi,” amesema Churkin pale Guterres alipoteuliwa mara ya kwanza.

Ban pia amemuita Guterres ni chaguo zuri kwa wadhifa wa katibu mkuu.

XS
SM
MD
LG