Umoja wa Ulaya umeongeza vikwazo dhidi ya serikali ya Syria Jumatatu na kupiga marufuku safari na kudhibiti mali za maafisa wengine watano wanaoaminika kuhusika na ukandamizaji wa raia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.
Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya Catherine Ashton alishutumu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya raia wa Syria na kusema kuwa ghasia za kikatili zimezusha mvutano na mgawanyiko katika nchi hiyo.
Umoja wa Ulaya haukutangaza majina ya maafisa wengine wa Syria waliolengwa kwenye vikwazo hivyo.
Marufuku hiyo inawahusu zaidi ya maafisa 30 wa Syria akiwemo rais Bashar al- Assad . Lakini wanaharakati wa Syria wanasema vifaru vya jeshi vilishambulia mji wa Hama kwa siku ya pili baada ya kuuwa takriban watu 80 katika mji huo jumapili.
Umoja wa Ulaya waongeza vikwazo Syria.

Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya Catherine Ashton alishutumu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya raia wa Syria