Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:32

Umoja wa Ulaya wamuondolea vikwazo waziri mkuu mpya wa Burundi


Waziri mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca
Waziri mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca

Umoja wa Ulaya umetangaza Jumanne kwamba umeondoa vikwazo dhidi ya maafisa watatu wa Burundi, akiwemo waziri mkuu mpya, ambaye alikuwa amewekewa vikwazo kutokana na jukumu lake katika mgogoro mbaya wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika ya kati.

Hatua hiyo ni ishara ya kufufua tena uhusiano kati ya Burundi na nchi za Magharibi chini ya uongozi wa Rais Evariste Ndayishimiye licha ya wasiwasi unaoendelea kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.

Uwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi umeandika kwenye Twitter “ Leo, EU imeondoa vikwazo binafsi dhidi ya watu watatu, akiwemo waziri mkuu Gervais Ndirakobuca.

Ujumbe huo umeongeza kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kuunga mkono juhudi na mageuzi ya maendeleo yanayofanywa na Burundi.

Ndirakobuca ambaye ni kamanda wa zamani wa waasi, ambaye aliwahi kuhudumu kama mkuu wa idara ya upelelezi na pia kama waziri wa usalama, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na Rais Ndayishimiye mapema mwezi Septemba.

Mzozo wa kisiasa wa mwaka 2015 ulipamba moto baada ya rais wa zamani Marehemu Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu.

Ndirakobuca alikuwa miongoni mwa maafisa waliotuhumiwa na Umoja wa Ulaya na Marekani kwa kuchochea ghasia dhidi ya wapinzani wa utawala.

XS
SM
MD
LG