Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 17:09

Umoja wa Ulaya waitoza faini ya dola bilioni 1.3 kampuni ya Meta kwa kuvunja sera ya kulinda data za siri


Nembo ya kampuni ya Meta inayomiliki mtandao wa Facebook.
Nembo ya kampuni ya Meta inayomiliki mtandao wa Facebook.

Umoja wa Ulaya Jumatatu umeitoza faini kubwa ya dola bilioni 1.3 kampuni ya Meta na kuiamuru isitishe kuhamisha data za wateja katika eneo la Atlantiki ifikapo mwezi Oktoba, ikiwa tukio la hivi karibuni katika kesi ya muongo mmoja iliyozushwa na hofu ya Marekani kuhusu udukuzi wa kidijitali.

Faini hiyo kuhusu taarifa za siri ya euro bilioni 1.2 iliyotolewa na tume ya Ireland ya kulinda data ndiyo faini kubwa tangu sera kali ya Umoja wa Ulaya kuhusu data za siri kuanza kutekelezwa miaka mitano iliyopita, na ikiwa juu ya adhabu ya euro milioni 746 dhidi ya kampuni ya Amazon kuhusu uvunjaji wa ulinzi wa data.

Taasisi hiyo ya Ireland ndiyo inasimamia shuguhuli ya ukaguzi wa taarifa za siri kwa kampuni ya Meta katika jumuia ya Umoja wa ulaya yenye nchi wanachama 27 kwa sababu makao makuu ya kampuni kubwa za teknolojia yako mjini Dublin.

Kampuni ya Meta, ambayo awali ilionya kuwa itafunga huduma kwa wateja wake barani Ulaya, imeapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kuiomba mahakama kusitisha uamuzi huo mara moja.

Kampuni hiyo ambayo inamiliki mtandao wa Facebook imesema “hakutakuwa na athari za mara moja kwa Facebook barani Ulaya.”

XS
SM
MD
LG