Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:48

Umoja wa Ulaya waipatia Zimbabwe msaada wa fedha


Picha ya Maktaba: Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Picha ya Maktaba: Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

Umoja wa Ulaya unaipatia Zimbabwe, karibu dola za kimarekani milioni 270.

Huo unakuwa msaada wa kwanza kwa serikali ya Rais Robert Mugabe, toka jumuiya hiyo ilipoiwekea Zimbabwe vikwazo mwaka 2002.

Msaada huo wa fedha ulitangazwa Jumatatu, Harare, Zimbabwe, na utahudumia sekta ya afya, kilimo na miradi ya utawala bora kwa kipindi cha miaka sita ijayo.

Kwa miaka mingi, Umoja wa Ulaya ulizuia misaada kwa Zimbabwe, lakini kupitia taasisi nyingine.

Vikwazo hivyo ni kutokana na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu wa maafisa wa Bwana Mugabe na washirika wake.

Kufuatia msukumo kutoka kwa mataifa ya Afrika, Umoja wa Ulaya uliweza kupunguza vikwazo vya kiusafiri na kifedha kwa baadhi ya maafisa wa Zimbabwe.

Lakini pamoja na yote hayo, vikwazo kwa Rais Robert Mugabe na mkewe bado vipo palepale.

XS
SM
MD
LG