Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:15

Viongozi wa Ulaya kukutana kwa ajili ya wahamiaji


People hold an European Union flag stained with red paint as they protest against the possible deal between the EU and Turkey to return thousands of migrants, in Madrid, Spain.
People hold an European Union flag stained with red paint as they protest against the possible deal between the EU and Turkey to return thousands of migrants, in Madrid, Spain.

Kwenye ajenda ya EU ni mpango ulio na utata kuwarudisha mamia ya wahamiaji Uturuki ili kuwapunguzia mzigo wa rasilimali nchi zilizoko ukanda wa mashariki wa Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajia kufikia makubaliano na Uturuki kuhusu wahamiaji katika mkutano wa siku mbili huko Brussels Alhamisi na Ijumaa.

Kwenye ajenda ni mpango ulio na utata kuwarudisha mamia ya wahamiaji Uturuki ili kuwapunguzia mzigo wa rasilimali nchi zilizoko ukanda wa mashariki wa Umoja wa Ulaya.

Kwa kila mkazi asiye na vibali vya kuishi ambaye Uturuki itampokea, Umoja wa Ulaya unasema utapokea mkimbizi mmoja wa Syria kutoka Uturuki. Umoja wa Ulaya unasema utachukua kufikia jumla ya kiasi cha wakimbizi 70,000 ambao watapatiwa makazi Ulaya katika hatua inayosimamiwa na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Taarifa ya pamoja juu ya jambo hilo inaita ni hatua ya kipekee naye aina yake kwamba ni muhimu kupunguza madhila ya binadamu na kurudisha amani.

XS
SM
MD
LG