Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 10:41

Umoja wa Ulaya wakubaliana juu ya mpango wa kupunguza gesi chafu


Maandamano ya kupinga ongezeko la uchafuzi wa mazingira.
Maandamano ya kupinga ongezeko la uchafuzi wa mazingira.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano yenye malengo makubwa ya kupunguza viwango vya gesi chafu kwa asilimia 55 ifikapo mwisho wa mwongo ikilinganishwa na viwango vya mwaka wa 1990 na hivyo kuepusha kikwazo kikubwa kabla ya mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa mwishoni mwa wiki hii.

Baada ya mazungumzo ya usiku mzima wakati wa kikao chao cha siku mbili mjini Brussells, nchi wanachama 27 za umoja wa ulaya leo zimeidhinisha pendekezo la tume ya utendaji ya umoja wa ulaya, kuzingatia lengo mbadala la umoja huo kwa kufikia viwango vya hewa safi ifikapo nusu karne.

Hayo ni baada ya nchi ambazo zinategemea sana mkaa wa mawe kuunga mkono lengo hilo lililoboreshwa.

Miaka mitano baada ya mkataba wa mjini Paris kuhusu hali ya hewa, Umoja wa Ulaya umesema unataka kuongoza katika vita dhidi ya viwango vya juu vya joto duniani.

Viongozi hao wamefanikiwa pia kufikia makubaliano juu ya bajeti yao na masaada wa kupambana na janga na virusi vya corona katika nchi zao.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, washington DC

XS
SM
MD
LG