Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:36

Umoja wa Mataifa yaadhimisha siku ya kimataifa ya walinzi wa amani.


Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wakisaidia katika mataifa yaliokumbwa na mzozo wa kisiasa.
Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wakisaidia katika mataifa yaliokumbwa na mzozo wa kisiasa.

Jumapili ilikuwa siku ya kimataifa ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wakikumbukwa zaidi ya wanaume na wanawake milioni moja kote duniani wanaovaa kofia za bluu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki- Moon alisema kofia za bluu zinaonyesha sifa ya wazi ya mshikamano ulimwenguni, ushujaa wa kutumika katika mazingira ya hatari na kuwapatia ulinzi baadhi ya watu walio katika mazingira hatari kote duniani.

Mapema mwezi huu Ban aliweka shada la maua nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani kuwakumbuka walinzi wa amani 3,400 ambao wamepoteza maisha yao tangu kuanza kwa opereshi ya kwanza ya ulinzi wa amani mwaka 1948.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema kwamba katika muda wa mwaka mmoja uliopita tume za ulinzi wa amani zimekabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuwapatia makazi raia 200,000 nchini Sudan Kusini wanaokimbia kuokoa maisha yao na timu ya ulinzi wa amani kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya kati kufanya uchaguzi wa rais kwa mafanikio.

XS
SM
MD
LG