Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 13, 2025 Local time: 10:25

Umoja wa Mataifa wazidi kuwa na wasiwasi na mashambulizi ya Gaza


Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu, Alhamisi amesema mashambulizi ya kijeshi ya Israel, katika Ukanda wa kusini wa Gaza ni marudio ya mashambulzi ya kaskazini mwa Gaza na kutoacha mahali popote salama kwa raia huku yakidumaza  shughuli za kibinadamu.

“Hatuna operesheni ya kibinadamu kusini mwa Gaza ambayo inaweza kufanyika tena,” Martin Griffiths aliwaeleza waandishi wa habari huko Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Amesema umekuwa mpango usiokuwa na uhakika wa kupata misaada ya kibinadamu na pale wanapoweza.

Amesema japo hilo ni la kushangaza na lisilo tegemewa japokuwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu hayata-waacha watu wa Gaza.

Israeli ilihamishia harakati zake za kijeshi kusini mwa Gaza Desemba 1, baada kuvunjika kwa makubaliano ya siku saba ya kusimamisha mapigano kupisha juhudi za kibinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG