Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:34

Umoja wa Mataifa watangaza njaa Somalia


Kinamama na watoto wa Kisomali wakisubiri misaada katika kambi moja ya waliokosa chakula nje kidogo ya Mogadishu, Somalia
Kinamama na watoto wa Kisomali wakisubiri misaada katika kambi moja ya waliokosa chakula nje kidogo ya Mogadishu, Somalia

Marekani imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya ukame katika eneo la pembe ya Afrika

Umoja wa Mataifa umetangaza rasmi kwamba kuna njaa katika maeneo mawili ya kusini mwa Somalia kufuatia kipindi cha ukame mkali kupata kutokea katika nchi hiyo katika muda wa miaka 50 iliyopita.

Akizungumza mjini Nairobi, msemaji wa Umoja wa Mataifa Mark Bowden alisema njaa imeingia katika maeneo ya Bakool na Lower Shabelle nchini Somalia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ametoa taarifa inayoelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya misaada ya dharura katika Pembe ya Afrika na tangazo hilo la Umoja wa Mataifa Jumatano.

Waziri Clinton alisema Marekani itatoa nyongeza ya dolla millioni 28 juu ya zaidi ya dolla millioni 431 katika misaada ya chakula na mahitaji mengineyo.

Shirika la Chakula duniani - FAO - limetoa wito wa dolla millioni 120 kwa ajili ya misaada ya eneo hilo kutoka jumuiya ya kimataifa. Zaidi ya nusu ya misaada hiyo itakwenda Somalia. Salio litakwenda katika nchi za Ethiopia, Kenya na Uganda.

XS
SM
MD
LG