Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:15

Umoja wa Mataifa wapongeza juhudi za amani Sudan

Sudan President Omar al-Bashir, right, arrives in Kigali, Rwanda, July 16, 2016, to attend an African Union summit. He defied an international warrant of arrest after public assurances from Rwandan leaders that he would not be arrested.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon siku ya Jumanne alipongeza mpango wa makubaliano ya kumaliza migogoro ya Sudan ulotiwa saini na vyama vya upinzani siku ya Jumatatu.

Mpango huo ulipendekezwa na jopo la utekelezaji la maafisa wa vyeo vya juu wa Umoja wa Afrika, na ulitiwa saini na serikali ya Sudan hapo tarehe 21 mwezi Machi mwaka huu.

Kupitia taarifa yake, Ban alisema amefurahia hatua iliyochukuliwa katika juhudi za kumaliza vita na kutanzua mizozo inayoendelea Sudan. Alitoa wito kwa wadau wote kuendelea kuunga mkono juhudi za kuafikiana, kwa kusitisha uhasama, kuhakikisha kwamba misaada inawafikia waathiriwa na kuunga mkono mkataba wa mwisho wa kisiasa ambao utapatikana kupitia mazungumzo ya kitaifa yatakayohusisha pande zote.

XS
SM
MD
LG