Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:41

Umoja wa mataifa waomba vikosi zaidi Ivory Coast


Askari wa umoja wa mataifa akifanya doria.
Askari wa umoja wa mataifa akifanya doria.

Umoja wa mataifa unasema unahitaji vikosi 1000 mpaka 2000 zaidi huko Ivory Coast kati kati ya ghasia za baada ya uchaguzi wakati rais aliyeko madarakani akikataa kuachia madaraka.

Kiongozi wa walinda amani wa umoja wa mataifa huko Ivory Coast Alain Le Roy alisema jumatano kuwa umoja wa mataifa utaliomba baraza la usalama kupata vikosi zaidi wakitumaini kwamba vitapelekwa katika wiki chache zijazo.

Walinda amani wamezunguka hoteli ambapo Alassane Ouattara mshindi anayetambuliwa kimataifa amezingirwa kwa wiki kadhaa.

Na Umoja wa mataifa unasemazaisdi ya watu 170 wameuwawa katika ghasia zilizolipuka tangu uchaguzi wa Novemba.

Juhudi za kumaliza mzozo huo zinaelekea kukwama licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika.

XS
SM
MD
LG