Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:12

Umoja wa mataifa waomba msaada kwa ajili ya Pakistan


Mafuriko makubwa huko Pakistani
Mafuriko makubwa huko Pakistani

Umoja wa mataifa umeomba karibu dola millioni 460 za misaada ya huduma

Umoja wa mataifa umeomba karibu dola millioni 460 za misaada ya huduma za dharura kutokana na janga kubwa la mafuriko ya maji huko Pakistan wakati ambapo wasi wasi unaongezeka kwamba wanamgambo wanaweza kutumia mzozo huo kwa maslahi yao.

Mafuriko yalianza mwezi uliopita huko kaskazini magharibi ambako jeshi la Pakistan limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Taliban wa Pakistan na wanamgambo wengine mnamo miaka miwili iliyopita.

Mpaka hivi sasa mafuriko yameuwa zaidi ya watu 1600 na kuwaathiri karibu milioni 14wengine katika majimbo ya Khyber-Pakhtunkwa, Punjab na Sindh. Mafuriko yanaelekea kuwa mabaya zaidi huko Kusini wakati mvua nyingi zaidi zinatabiriwa kwenye eneo hilo.

XS
SM
MD
LG