Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 23:37

Umoja wa mataifa wamtambua Outtara kama rais Ivory Coast


Vikosi vya umoja wa mataifa katika mitaa ya Abidjan.

Baraza kuu la Umoja wa mataifa limemtambua Alassani Ouattara kama mshindi wa uchaguzi mkuu wa rais wa Ivory Coast.

Baraza hilo lenye nchi wanachama 192 duniani lilipitisha muswaada Alhamisi wa kumpitisha mteule wa Bw. Ouattara kwenye nafasi ya ubalozi wa nchi hiyo kwenye umoja wa mataifa.

Hatua hiyo inampa nguvu Bw. Ouattara katika juhudi zake za kumuondoa Laurent Bagbo ambaye amekataa kuachia madaraka baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita uliopingwa.

XS
SM
MD
LG