Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:44

Umoja wa Mataifa walaumiwa kwa Kipindupindu nchini Haiti


Daktari akihudumia wagonjwa wa Kipindupindu Haiti
Daktari akihudumia wagonjwa wa Kipindupindu Haiti

Taasisi ya haki na demokrasia ya Haiti iliwasilisha rasmi malalamiko katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jumanne

Mawakili wanaowakilisha waathiriwa wapatao elfu tano wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Haiti wamewasilisha malalamiko yao rasmi kwa Umoja wa Mataifa, wakidai mamilioni ya dola kama fidia kwa waathiriwa na wanataka shirika hilo la kimataifa liombe msamaha. Mlipuko huo wa Kipindupindu yaaminika ulitokana na walinda amani wa Umoja wa Mataifa raia wa Nepal na kuuwa wahaiti elfu sita na mia sita tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Taasisi ya haki na demokrasia ya Haiti iliwasilisha rasmi malalamiko hayo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki jana na kupeleka nakala nyingine kwa tume ya Umoja wa Mataifa huko nchini Haiti inayojulikana kama MINUSTAH. Kundi hilo linasema Umoja wa Mataifa na tume yake huko kisiwani MINUSTAH, yanawajibika kwa mlipuko wa kipindupindu kwa kushindwa kuwakagua vyema walinda amani wake waliotoka katika nchi zilizokumbwa na mlipuko wa ugonjwahuo. Brian Concannon wakili katika taasisi hiyo ya haki na demokrasia aliwaambia waandishi habari jana kuwa wanataka fidia kutoka kwa Umoja wa Mataifa.Taasisi ya haki na demokrasia huko Haiti inasema inatumai kukutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa kujadilia malalamiko hayo. Mawakili wa kundi hilo wamesema watafuatilia swala hilo katika mahakama ya Haiti au New York ikiwa hawatafikia maelewano na Umoja wa Mataifa. Wanasema haitawezekana kwa Umoja wa Mataifa kutumia kinga yake kama shirika la kimataifa katika swala ambalo walinda amani wake wamepeleka maradhi katika nchi.

XS
SM
MD
LG