Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:35

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la Helikopta ya walinda amani DRC


Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi la Februari 5, dhidi ya helikopta na kikosi cha kulinda amani cha umoja huo (MONUSCO) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres imesema kuwa helikopta hiyo ilishambuliwa wakati ikisafiri kutoka Beni kuelekea Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, na kupelekea mlinzi mmoja wa amani raia wa Afrika Kusini kuuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya sana. Wanahewa wengine walifanikiwa kuta na helikopta hiyo mjini Goma.

Katibu Mkuu alielezea masikitiko yake mkubwa kwa familia ya mlinzi wa amani aliyepoteza maisha pamoja na familai yake na watu wa Jamhuri ya Afrika Kusini. Pia alisema anamuombea mwanajeshi aliyejeruhiwa kupata afueni ya haraka.

Katibu Mkuu amekumbushia mashambulizi dhidi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huenda yakapelekea kuwa ni uhalifu wa kivita kwa mujibu wa sheria ya kimataifa. Ameitaka mamlaka ya Congo kuchunguza shambulizi hili la kinyama na haraka kuwawajibisha mbele ya sheria wahusika.

Katibu Mkuu amethibitisha tena kwamba Umoja wa Mataifa, kupitia mwakilishi wake maalum huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wataendelea kuisadia serikali ya Congo na watu wake katika juhudi zao za kuleta amani na uthabiti mashariki mwa nchi hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG