Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:27

UN yachunguza shutuma za ngono jamhuri ya Afrika ya kati


Ujumbe wa walinda amani wa umoja wa mataifa.
Ujumbe wa walinda amani wa umoja wa mataifa.

Umoja wa Mataifa unachunguza shutuma mpya mbaya za unyanyasaji wa kijinsia na dhulma ya mapenzi zinazoelekezwa kwa walinda amani wake wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Toka kundi la utetezi lenye makazi yake hapa Marekani la “AIDS-Free Worlds Code Blue Campaign,” kuifahamisha Umoja wa Mataifa, walinda amani kutoka nchini Burundi na Gabon wamezuiliwa makambini wakati uchunguzi ukiendelea.

Kundi hilo linasema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na vikundi vyenye silaha pia vilishiriki katika makossa hayo kwa karibu wasichana 98 katika kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013.

Shutuma hizo pia zimeelekezwa kwa vikosi vya Ufaransa vya Sangaris.

XS
SM
MD
LG