Israel inasema matamshi hayo ni propaganda ya kundi la Hamas.
Katika taarifa ya pamoja waatalamu hao wanasema wana imani kwamba watu wa Palestina wako katika hatari kubwa ya mauwaji ya kimbari.
Wameongeza kusema kwamba washirika wa Israel pia wanabeba mzigo wa kuwajibika na ni lazima wachukuwe hatua za haraka na dharura sasa hivi kuzuia janga hilo kukamilika.
Waatalamu hao wanasema hali huko Gaza imefikia kilele cha janga kubwa, wakionya juu ya upungufu mkubwa wa maji, chakula dawa, mafuta na vifaa muhimu vya msingi pamoja na hatari ya milipuko ya ugonjwa.
Ujumbe huo wa watalaamu wa haki za binadam wanatoa kusitishwa na mashambulizi ili kuruhusu msaada wa dharura uweze kuingia kwenye ukanda huo.
Israel imedondosha mabomu makubwa na mengi kwenye ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa Hamas kufanya shambulio la kipekee kuwahi kutokea mwezi uliyopita.
Forum