Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 04:38

Umoja wa mataifa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Sudan.


Askari wa Sudan akiangalia eneo la Kordofan kusini.
Askari wa Sudan akiangalia eneo la Kordofan kusini.

Rasimu ya azimio inaeleza bara la usalama linaweza kuchukua hatua zisizo za kijeshi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupitisha azimio Jumatano linaloitaka Sudan na Sudan Kusini kusitisha mapigano na kutatua masuala yao yaliopo au kukabiliwa na uwezekano wa vikwazo. Rasimu ya azimio iliyoipata Sauti ya Amerika inazitaka pande zote mbili kuacha mara moja uhasama wote na kufikia mkataba juu ya masuala ya mafuta, mpaka na uraia. Rasimu hiyo inaelezea umuhimu wa kurejesha amani kamili na ya kudumu kati ya Sudan na Sudan Kusini. Rasimu hiyo inasema kama upande wowote unashindwa kufuata azimio hilo, baraza la usalama litachukua hatua chini ya kipengele cha 41 cha kanuni za Umoja wa Mataifa. Kipengele hicho kinairuhusu baraza hilo kuchukua hatua zisizo za kijeshi, ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ili kuunga mkono uamuzi wake.

XS
SM
MD
LG