Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:13

UAE yasema haijamaliza jukumu lake na Yemen


watoto wakicheza katika jengo lililobomoka baada ya mashambulizi ya anga ya saudi arabia

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umeeleza leo Ijumaa kwamba jukumu lake katika vita nchini Yemen halijakwisha, tofauti na taarifa iliyotolewa siku moja kabla ambayo ilielezea kujitoa.

Mfalme wa Abu Dhabi alituma taarifa kutoka Waziri wa Mambo ya Nje, Anwar Gargash, kwenye mtandao wake wa kiofisi kwamba vita nchini Yemen vimekwisha kwa wanajeshi wake baada ya kuwa mshirika mkuu katika ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia kupambana na waasi wanaoungwa mkono na Iran kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Taarifa iliyo katika lugha ya Kiarabu, hata hivyo inasomeka kwamba vita vimekwisha kwa vitendo pekee.

Gargash aliviambia vyombo vya habari leo Ijumaa kwamba taarifa ilichukuliwa vibaya na haielezei ukweli.

XS
SM
MD
LG