Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:27

Umoja wa Falme za Kiarabu watuma magari ya kijeshi na zana nyingine nchini Chad


Waandamanaji wanaoipinga serikali walichoma kizuizi wakati wa mapigano huko N'Djamena, Chad, Alhamisi Oktoba 20, 2022. AP
Waandamanaji wanaoipinga serikali walichoma kizuizi wakati wa mapigano huko N'Djamena, Chad, Alhamisi Oktoba 20, 2022. AP

Umoja wa Falme za Kiarabu umetuma magari ya kijeshi na zana nyingine za usalama nchini Chad kuunga mkono juhudi za kupambana na ugaidi na ulinzi wa mpaka, nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta ya Ghuba ilisema Jumapili.

Chad ni jirani wa Niger ambako mapinduzi ya mwishoni mwa mwezi uliopita yalimuondoa madarakani kiongozi mmoja wa mwisho anayeungwa mkono na viongozi wa Magharibi katika eneo linalokumbwa na ugaidi la Sahel.

Shirika rasmi la habari la UAE WAM lilionyesha picha za magari kadhaa ya kivita yenye rangi ya jangwani huku bendera za Imarati na Chad zikiwa zimepambwa juu ya magari mawili kati ya hayo. Kampuni ya Imarati ya NIMR inatengeneza magari hayo.

WAM imesema nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi mwezi Juni wakati wa ziara ya rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno ambaye ameongoza nchi hiyo tangu baba yake Idriss Deby Itno alipofariki dunia kutokana na majeraha yaliyompata baada ya kupambana na waasi zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Forum

XS
SM
MD
LG