Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:32

Umakini wa Rwanda katika bajeti ndio unaokuza uchumi


Wachumi wanasema Rwanda imeweza kufanya vyema kwenye uchumi kutokana na kuwa makini kwenye matumizi ya bajeti yake.

Licha ya hayo baadhi yao wanasema kuagiza bidhaa ghafi kutoka nchi za kigeni kumesababisha kudorora kwa sarafu yake dhidi ya dola ya Marekani.

Mwandishi wa idhaa hii Sylivanus Karemera wa Kigali, Rwanda, aliongea na wataalamu wa uchumi baada ya Rwanda kutangaza makadirio ya bajeti yake sambamba na nchi nyingine za jumuiya ya Afrika.

Faranga trilioni 1.94 zimetengwa kwa mwaka 2016/17 ikiwa ni ongezeko la Faranga bilioni 140 ikilinganishwa na bajeti iliyopita.

Waziri wa fedha wa Rwanda Claver Gatete amesema kwa mara ya kwanza asilimia 64% ya bajeti hii itatokana na makusanyo ya ndani huku asilimia 36% iliyobaki ikitoka kwenye mikopo na misaada ya wahisani.

Sekta ya ujenzi hasa wa barabara mpya, huduma za jamii, usafiri na usafirishaji zimetengewa kiasi kikubwa cha fedha ikiwa ni asilimia 40% ya bajeti nzima.

Stephen Ineget wa kampuni ya kimataifa ya KPMG amesema sababu inayoifanya kutekeleza miradi yake ya maendeleo iliyopangwa katika bajeti ni kwa sababu ya kusimamia vizuri fedha zake.

Imetangazwa pia kwamba sarafu ya Rwanda imepungua kwa asilimia 7.6 dhidi ya dola ya Marekani, huku uchumi ukitarajiwa kukua kwa kiwango cha asilimia 6.4% mwaka 2016/2017.

Profesa Thomas Kigabo kutoka benki kuu ya Rwanda amesema kuporomoka kwa faranga ya Rwanda dhidi ya dola ni suala ambalo tulilitarajia.

Profesa Kigabo amesema ukiangalia kwa miaka 10 iliyopita uchumi umekuwa kwa kasi ya juu hali iliyosababisha kuagizwa malighafi nyingi kutoka nje ya nchi kitu kilicho ongeza mahitaji ya Marekani huku bidhaa za ndani zinazouzwa nje ya nchi ni chache.

Pamoja na masuala hayo imeelezwa hakuna athari katika ukuwaji wa uchumi kwa kiwango cha asilimia 6.5 kwa mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:14 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG