Wanaharakati wa Sudan wanaounga mkono demokrasia waliandamana kupinga jeshi na wanamgambo siku ya Alhamisi wakati upinzani wa kiraia ukiadhimisha kumbukumbu kuu ya mapambano ya miongo kadhaa dhidi ya utawala wa kijeshi kwa maandamano mapya.
Uchelewesho mpya wa kusainiwa kwa makubaliano ya kuirejesha serikali ya kiraia, ambako kulikuwa kumepangwa tena Alhamisi, kulisababisha upinzani wa kiraia kuitisha maandamano ya nchi nzima.
Turk, kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, alizitaka pande zote kupunguza mivutano isisambae na kujiepusha na ghasia kwa kuwa hatua kubwa zimepigwa mpaka sasa ili kurejesha mageuzi ya kisiasa kwa njia sahihi.