Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:33

UM umejiandaa endapo ghasia zitazuka nchini DRC


Umoja wa mataifa unafanya mipango ya dharura kushughulikia ongezeko la haraka la mahitaji ya misaada ya kibinadamu endapo hali ya kisiasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itageuka na kuwa ghasia.

Umoja wa mataifa umekuwa ukionya kwa miezi kadhaa kwamba bila kuwepo kwa mazungumzo ya kina ya kitaifa, mivutano nchini DRC inaweza kujitokeza na kuendelea na kuna uwezekano ikageuka kuwa ghasia.

Umoja wa mataifa una walinda amani 20,000 nchini humo hasa katika eneo tete la mashariki na imekuwa ikifanya mipango ya dharura ya kijeshi ili kuwalinda raia kama hali hiyo itaongezeka.

Siku ya Jumanne, mratibu mkazi wa tume ya kibinadamu, Mamadou Diallo, ameliambia kundi dogo la mataifa wanachama kwamba timu yake pia inajiandaa kama kutatokea ghasia zinazo husiana na uchaguzi ama watu kukosa makazi.

DRC imekuwa ni nchi inayotegemea juhudi za misaada ya kibinadamu kwa miongo miwili iliyopita, kutokana na ghasia za ndani na majanga ya asili, na kuwafanya wananchi wake kugeuka kuwa wakimbizi.

Kwa sasa, Diallo amesema nchi hiyo inapambana na homa ya manjano pamoja na kipindipindu, na ipo mbioni kutokomeza mlipuko wa surua.

Umoja wa mataifa umeomba karibu dola milioni 700 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini DRC kwa mwaka huu lakini imefanikiwa kupokea nusu yake na kusaidia takriban watu milioni 6.

Dialloa amesema karibu Wakongo milioni 8 watahitaji misaada hapo mwak

XS
SM
MD
LG