Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 13:32

UM kuratibu mchakato wa uchaguzi wa Libya


Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Stephanie Koury.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Stephanie Koury.

Umoja wa Mataifa utaitisha kamati ya ufundi ya wataalamu wa Libya kutatua masuala mazito na kuiweka nchi hiyo kwenye mwelekeo wa uchaguzi wa kitaifa unaosubiriwa kwa muda mrefu, kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) amesema Jumapili.

Mchakato wa kisiasa wa kutatua mzozo wa zaidi ya muongo mmoja nchini Libya umekwama toka uchaguzi uliopangwa kufanyika Disemba 2021 kushindikana huku kukiwa na mizozo kuhusu uhalali wa wagombea wakuu.

Kamati mpya ya wataalam wa Libya itaangalia njia za kukabiliana na masuala ambayo hayajakamilika katika sheria za uchaguzi, kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa (UNSMIL), Stephanie Koury, amesema katika taarifa yake ya video.

Alisema pia watatafuta njia za kufikia uchaguzi katika muda mfupi iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na dhamana na muda uliopendekezwa.

Forum

XS
SM
MD
LG