Imeongeza kusema wakiwa huko wataendelea kutoa misaada ya kuokoa maisha licha ya marufuku ya Taliban ya ajira kwa wanawake wa Afghanistan katika mashirika yasiyo ya kiserikali.
"Jumuiya ya kibinadamu haifanyi mgomo," Martin Griffiths, afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu, aliwaambia wawakilishi wa nchi wanachama siku ya Jumatano.
Tangazo hilo linakuja wakati baadhi ya mashirika ya misaada ya kimataifa kuamua kusitisha shughuli zao nchini Afghanistan kupinga agizo la Desemba 24, 2022, la serikali ya Taliban kupiga marufuku wanawake wa nchini humo kufanya kazi kwenye mashirika yasiyo ya kiserekali.