Katika tamko hilo lililotolewa Jumamosi, Chama cha Wanasheria Uganda (ULS) kimesema kuwa japokuwa Bunge linauwezo wa kuendesha mchakato huo wa kurekebisha kifungu cha Katiba namba 102, katika ari ya kuipa kipaumbele katiba zoezi hili lazima liwashauri wadau na wananchi mbalimbali.
“Hatua za kurekebisha Katiba ni lazima iruhusu ushauri mpana na kuwashirikisha wananchi, na haki za wananchi wa Uganda kukusanyika kwa amani, kuandamana na kueleza maoni yao lazima iheshimiwe na kulindwa na polisi,” amesema rais wa ULS, Francis Gimara.
Amesema kanuni ya msingi na muundo wa Katiba ya mwaka 1995 inatakiwa ipewe umakini wa kutosha ili kuepuka hali ya kuyumba kisiasa na kasoro za kikatiba.
Kauli ya wanasheria imekuja wakati kukiwa na mgogoro nchi nzima juu ya mswada uliopelekwa bungeni kutaka kurekebishwa kwa kifungu 102(b) ambacho kinaainisha umri wa chini wa miaka 35 na umri wa juu wa miaka 75 kuwa ndio kigezo cha mgombea wa urais kuruhusiwa kugombea.
Kwa mujibu wa Gimara, mjadala huo ndani na nje ya Bunge umeibua masuala kadhaa yanayohusiana na Utawala wa Sheria, Ukatiba, na kushirikishwa wananchi katika kupata viongozi wao.
Facebook Forum