Marufuku hiyo inajiri sambamba na bei ya kikomo iliyokubaliwa na kundi la nchi 7 washirika wa Ulaya.
Lengo ni kuruhusu mafuta ya dizeli yaendelee kusafirishwa kwa wingi katika nchi kama China na India na kuepuka kupanda ghafla kwa bei ambako kutaathiri wanunuzi duniani kote, huku marufuku hiyo ikipunguza mapato yanayofadhili bajeti na vita vya Moscow.
Mafuta ya dizeli ni muhimu kwa uchumi wa Russia kwa sababu yanatumiwa na gari, malori yanayobeba bidhaa, vifaa vya kilimo na mashine za viwanda.